Dar es salaam || Akizungumza katika Kongamano lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kupitia Kigoda cha Uprofesa cha Mwalimu J.K. Nyerere katika Taaluma za Umajumui wa Afrika, kwa kushirikiana na Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP), Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia nchini (PPPC), Bwana David Kafulila, amesema kuwa ili kukuza uchumi jumuifu ni lazima kuwekeza nguvu katika sekta zinazogusa wananchi wengi kwa wakati mmoja.
Kafulila akirejelea ripoti ya REPOA ya mwaka 2008 inayobainisha kuwa “ukikuza kilimo kwa asilimia 8–10 kwa miaka mitatu mfululizo, unaweza kupunguza umasikini kwa asilimia 50.” Amesema matokeo chanya yanayoonekana sasa yametokana na interventions mbalimbali za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia, ambazo zimebadilisha mwenendo wa kilimo, mifugo na uvuvi katika kipindi cha miaka minne.
Kafulila pia alisisitiza umuhimu wa ushiriki wa sekta binafsi, akisema kuwa tukiruhusu sekta binafsi kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya kilimo, mifugo, uvuvi na misitu, tutakuwa na uwezo wa kufanya vizuri zaidi na kuongeza tija ya sekta hizi kwa kiwango kikubwa.
Aidha, Kafulila alibainisha kuwa kuna mambo manne muhimu yanayochochea maendeleo ya nchi: Human Capital (watu wenye ujuzi na elimu), Geographical Position (nafasi ya kijiografia), Natural Resources (rasilimali asili) na Diplomatic Relations (ushirikiano wa kidiplomasia). Akizungumzia zaidi nafasi ya kijiografia, Kafulila alisema kuwa Tanzania ina nafasi ya kipekee kwa kuzungukwa na nchi zisizo na bandari, huku zaidi ya asilimia 80 ya biashara yote duniani ikifanyika kupitia bandari. Amesisitiza kuwa Bandari ya Kilwa ni bandari bora zaidi Afrika Mashariki na Kati, ikitoa fursa kubwa ya biashara na uwekezaji wa kimataifa, ukiongeza ufanisi na mapato ya taifa.
Sekta ya Kilimo
Kafulila amesema bajeti ya wizara imeongezeka kutoka Sh. bilioni 294 mwaka 2021 hadi Sh. trilioni 1.242 mwaka 2025. Kupitia interventions za upatikanaji wa pembejeo, mbolea imeongezeka kutoka tani 678,017 mwaka 2021 hadi tani 1,213,780 mwaka 2024, huku Serikali ikitoa ruzuku ya Sh. bilioni 708.6. Aidha, ujenzi wa kiwanda cha mbolea cha ITRACOM Dodoma chenye uwezo wa kuzalisha tani 1,000,000 kutamaliza kabisa tatizo la upungufu wa Mbolea nchini.
Katika eneo la umwagiliaji, Kafulila ameeleza kuwa maeneo yameongezeka kutoka hekta 561,383 mwaka 2020/21 hadi hekta 1,270,647.06 mwaka 2025/26. Interventions hizi zimechangia uzalishaji wa chakula kuongezeka kutoka tani milioni 17.1 mwaka 2021 hadi tani milioni 22.8 mwaka 2024.
Sekta ya Mifugo na Uvuvi
Akieleza kuhusu sekta ya mifugo na uvuvi, Kafulila amesema Idadi ya viwanda vya kuchakata nyama vimeongezeka kutoka vitatu hadi saba.Akizungumzia uvuvi, Kafulila amesema mauzo ya nje ya mazao ya sekta hiyo yameongezeka na Mafanikio hayo yamechochewa na interventions mbalimbali ikiwemo ujenzi wa Bandari ya Uvuvi Kilwa kwa gharama ya Sh. bilioni 279.5, ambayo kwa mujibu wa Kafulila ni bandari bora zaidi Afrika Mashariki na Kati. sasa msikilize mpaka mwisho.