RAIS SAMIA KUMALIZA UHABA WA WALIMU NAMTUMBO ENDAPO ATACHAGULIWA.
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewaomba wananchi wa wilaya ya Namtumbo wamchague yeye pamoja na wagombea wengine wa CCM ili serikali iendelee kuboresha sekta ya elimu katika eneo hilo. Akihutubia maelfu ya wananchi, Dkt. Samia alieleza kuwa iwapo atachaguliwa tena, serikali yake itajiri walimu 7,000 nchini, na baadhi yao watapangiwa wilayani Namtumbo ili kupunguza changamoto ya upungufu wa walimu. Aidha, ameahidi kuwa wanafunzi wote wanaosoma shule za umma wataendelea kunufaika na sera ya elimu bure, ili kuhakikisha kila mtoto anapata fursa sawa ya kujifunza bila kikwazo cha ada.

