DKT. SAMIA AAHIDI NEEMA KWA WAKULIMA TUNDURU ENDAPO ATASHINDA.

Published:

Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM,

Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewahakikishia wananchi wa wilaya ya Tunduru kuwa serikali yake iwapo itachaguliwa tena akatika uchaguzi mkuu ujao  itaendelea kulipa kipaumbele sekta  kilimo kwa kuwa ndicho uti wa mgongo wa mkoa huo na taifa kwa ujumla.

Dkt. Samia Ameeleza kuwa  katika kipindi kilichopita serikali yake iliongeza  skimu 20 za umwagiliaji. Mhe Samia amewahidi kuwa sekta ya kilimo ni kipaumbele chake ndio sababu ilani ya 2025-2030 kitaifa  imelenga kuongeza eneo la skimu ya umwagiliaji kutoka hekta milioni 1.2 hadi milioni 5, ongezeko la eneo la umwagiliaji itawezesha wakulima kuongeza wigo wa uzalishaji kwa kuwa wataweza kulima zaidi ya msimu mmoja.

Aidha, ameahidi kujenga soko la kisasa, kuanzisha maghala matatu ya kuhifadhia mazao, pamoja na vituo vya zana za kilimo vitakavyowawezesha wakulima kuongeza tija na kuinua kipato chao.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img