DKT. SAMIA KUWANUFAISHA WAKULIMA NAMTUMBO ENDAPO ATACHAGULIWA. 

Published:

 Mgombea kiti cha urais kupitia CCM amewaomba wakulima  wa wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma kuwachagua wagombea wanaotokana na CCM akiwemo yeye katika nafasi ya Urais  katika uchaguzi mkuu ujao ili ainue sekta ya kilimo.

  Dkt. Samia amesema serikali ya CCM itaandaa mazingira bora ya kuboresha zao la tumbaku, ambalo ni uti wa mgongo  kwa wakulima wa Namtumbo na maeneo jirani. Ameeleza kuwa chama hicho, kupitia ilani ya uchaguzi wa 2025–2030, kitaendelea kutoa ruzuku ya mbolea ili kupunguza gharama za uzalishaji na kuwawezesha wakulima kuongeza tija na kipato.

Amesisitiza kuwa sera hizi zinalenga kumuinua mkulima mdogo na kuhakikisha Ruvuma inanufaika zaidi na rasilimali zake. Katika hatua nyingine Mhe. Dkt Samia ameahidi kumega na kurejesha ekari 3000 kutoka NAFCO kwa wananchi, amesema kuwa eneo hili litatumika mahususi kuzalisha mbegu bora ambapo itapunguza uagizaji wa mbegu kutoka  nje ya nchi. 

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img