SASA DKT. SAMIA KUIFUNGUA SONGEA KIUCHUMI ENDAPO ATASHINDA

Published:

Mgombea wa urais kupitia CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewaahidi wananchi wa Songea kuwa endapo atachaguliwa kwenye uchaguzi mkuu ujao ataifungua Ruvuma kimawasiliano na kimaendeleo. Ametaja miongoni mwa vipaumbele vyake kuwa ni kukamilisha uwanja wa ndege wa Songea kwa kujenga jengo la kisasa la abiria na kukarabati njia za kurukia ndege, ili kuongeza fursa za biashara na utalii. Pia ameahidi kukamilisha Bandari ya Bambabay, ambayo tayari imefikia asilimia 35 ya ujenzi, sambamba na hili Dkt. Samia ameeleza dhamira ya kufanikisha ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR kutoka Mtwara hadi Bambabay, hatua itakayofungua ukanda wa kusini kimaendeleo. Aidha, ametangaza mpango wa kujenga barabara ya kupita nje ya mji wa Songea (Bypass) ili kupunguza msongamano na kurahisisha usafiri wa ndani.

“Tutahakikisha Mawasiliano Ya Simu Yanapatikana Kila Mahali Songea Ahadi Ya  Dkt. Samia “

Mgombea wa Urais kupitia CCM Dkt. Samia ameahidi kuboresha upatikanaji wa huduma za simu mkoani Ruvuma. Amesema CCM  ikichaguliwa tena kushika dola itahakikisha maeneo yote ambayo kwa sasa hayana mawasiliano ya uhakika yanafikiwa na huduma hizo, ili wananchi waweze kuwasiliana kwa urahisi na kunufaika na fursa mbalimbali za kijamii na kiuchumi.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img