CCM kupitia mgombea wa kiti cha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imewaahidi wananchi katika wilaya ya Songea endapo watakipa ridhaa tena chama cha Mapinduzi katika uchaguzi mkuu ujao itawajengea wafanyabishara ndogondogo (machinga) soko la kisasa katika maeneo ya Manzese A na B katika wilaya Songea.
Dkt. Ameleza kuwa ni azma yake kurasimisha sekta hii muhimu inahusisha wananchi wengi hususan vijana. Dkt Samia ameeleza kuwa endapo wananchi wa Songea watamchagua atahakikisha atajenga soko hilo la kisasa ili machinga wafanye biashara zao katika mazingira yenye staha na kuwaomba wananchi wamchague ili kuwaletea maendeleo.

