Akiwa Wilayani Nanyumbu, Dkt. Samia amewaahidi wananchi kuendelea kuboresha barabara za lami ndani ya mji wa Mangaka na zile zinazounganisha wilaya na mkoa ikiwa ni pamoja na kujenga madaraja pale yanapohitajika.
Hata hivyo, ameeleza kuwa changamoto za wanyama waharibifu kwenye maeneo yanayozunguka misitu ya Lukwila na Lumesule zitapatiwa ufumbuzi.
Aidha, amesisitiza kuwa serikali yake itaongeza maeneo rasmi ya malisho kwa wafugaji kutoka Hekta milioni 3.4 za sasa hadi kufikia hekta milioni 6 ifikapo mwaka 2030.

