TUMENUNUA DRONE 5 KUPAMBANA NA WADUDU WAHARIBIFU WA MAZAO-DKT SAMIA

Published:

AKIWA KATA YA NAKAPANYA WILAYA YA TUNDURU MKOA WA RUVUMA

Kwanza, Dkt Samia alizungumzia pia kuhusu huduma Za Kijamii

Dkt. Samia Suluhu Hassan amehutubia wananchi wa Nakapanya, akiahidi kujenga kituo cha afya katika kata ya Namiungo ambacho hakikukamilika awamu iliyopita. Aidha, amesisitiza kuwa vituo vya afya na zahanati ambavyo bado havijakamilika, vitakamilishwa ili kuongeza upatikanaji wa huduma za afya.

Kwenye sekta ya maji, mgombea wa chama cha mapinduzi ameahidi kuhakikisha kuwa kila mwananchi anapata maji safi na salama

Aidha, amesisitiza kuwa umeme sasa umefika vijiji vyote, na hatua inayofuata ni kuunganisha vitongoji vyote.

Pili, Dkt Samia pia amezungumzia Kilimo na Umwagiliaji

Dkt Samia ameeleza kuwa serikali itaendeleza ruzuku ya mbolea na pembejeo, pamoja na kujenga skimu za umwagiliaji na mabwawa ili wakulima wazalishe mara mbili kwa mwaka, ukilinganisha na mara moja kufuatia mvua. Aidha, amesema kuwa serikali imenunua ndege zisizokuwa na rubani (drones) tano kwa ajili ya kukabiliana na changamoto za wanyama waharibifu, na zitapelekwa maeneo yenye changamoto kubwa.

Tatu, Dkt Samia amezungumzia bei za Mazao

Kwa upande wa bei za mazao, ameeleza kuwa serikali ipo kwenye mazungumzo na masoko makubwa, ikiwemo India, kuhakikisha bei hazishuki zaidi ya asilimia 60 ya bei ya dunia, ili kulinda kipato cha wakulima.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img