RAIS SAMIA APELEKA KICHEKO CHA BANDARI YA KASANGA RUKWA, MKOA WATAMANI PPP UJENZI WA MELI ZA KISASA.

Published:

Chini ya uongozi wa Serikali ya Rais Samia, Bandari ya Kasanga mkoani Rukwa imekarabatiwa kwa shilingi bilioni 20 (dola milioni 8) chini ya Serikali ya Rais Samia, ikiwa na uwezo wa meli 4 kutia nanga kwa wakati mmoja na kuhudumia abiria 800 kwa siku (292,000 kwa mwaka), huku ikitarajiwa kutoa ajira 200 za moja kwa moja na 600 zisizo za moja kwa moja.

TPA inatekeleza mradi huu kwa shilingi bilioni 4.76 kwa fedha za ndani kwa ajili ya upanuzi wa gati kutoka mita 20 hadi 120, ujenzi wa jengo la kupumzikia abiria na nyumba za wafanyakazi.

viongozi wa mkoa wamependekeza Serikali kushirikiana na sekta binafsi (PPP) kujenga meli kubwa za mizigo zitakazovusha malori moja kwa moja kwenda DRC na Zambia bila kupitia Tunduma, ili kupunguza msongamano na gharama za usafiri; bandari hii ni ya kimkakati, ina uwezo wa kuhudumia nchi nyingi kupitia Ziwa Tanganyika, na ni sehemu ya juhudi za kitaifa kuboresha miundombinu ya usafirishaji wa majini kwa mikoa ya kusini-magharibi ya Tanzania.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img