Mgombea kiti cha Urais kupitia CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan amewaomba wananchi wa mji wa Songea kujitokeza kwa wingi na kukipigia kura chama cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi oktoba mwaka huu ili kufanikisha ujenzi wa kongani ya viwanda katika wilaya ya Songea.
Mhe. Dkt. Samia ameeleza kuwa iwapo atachaguliwa na wananchi wa Songea mjini serikali ya CCM itahakikisha inatengeneza mazingira mazuri ya kuvutia wawekezaji watakaowekeza katika ujenzi wa kongani ya viwanda ili kuongeza tija katika mazao hasa mazao ya misitu na parachihi ambapo utasaidia kupunguza changamoto ya ukosefu wa ajira katika wilaya ya Songea.
Sambamba na hili Mhe. Dkt Samia ameahidi kuwa serikali ya CCM atakayoiongoza itanunua mitambo ya kukuboa kawaha. Katika hatua nyingine Dkt. Samia ameahidi kuanzisha kongani ya viwanda wa madini ili kuwezesha kuongeza wigo wa uchimbaji kwa wachimbaji wadogo.
“KUMCHAGUA DKT SAMIA NI KUCHAGUA RUZUKU YA PEMBEJEO ZA MBOLEA NA MBEGU-SONGEA/ RUVUMA“
Chama cha Mapinduzi kupitia mgombea wake wa Urais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameahdi wananchi wa wilaya ya Songea na mkoa wa Ruvuma ataongeza wigo wa upatikanaji wa mbolea ya ruzuku kwa wakulima katika wilaya hiyo,mbali na ruzuku Mhe. Samia ameahidi kuongeza huduma za ugani kwa wakulima ili wazalishe kwa ubora na tija
Mhe. Dkt. Samia ametoa ahadi ya kuanzisha mashamba ya kiwanda sukari katika halmashauri ya wilaya ya Peramiho, Katika hatua nyingine Mgombea wa Urais amewasihi wakulima wa wilaya wa Songea kuepuka kuuza mbolea wanazopewa kwa ruzuku kwa wafanyabishara wasio waaminifu badala yake wazitumie kuongeza uzalishaji na ubora kwa mazo yao.

