Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika ziara ya kampeni mkoani Ruvuma, amewaomba wananchi wa Wilaya ya Tunduru kumchagua tarehe 29 Oktoba, ili serikali yake iendelee kuimarisha huduma za afya nchini.
Katika hotuba yake, Dkt. Samia ameahidi kujenga zahanati 20 na vituo vya afya 3 katika Wilaya ya Tunduru, ikiwa ni sehemu ya mpango wa kitaifa wa kujenga zahanati 947 na vituo vya afya 277 kote nchini.
Aidha, Mhe. Samia ameahidi kuwa endapo atachaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, serikali ya CCM itaanza mara moja utekelezaji wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote, ili kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma za matibabu bila kikwazo cha gharama.

