Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewaomba wananchi wa wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma wamchague yeye pamoja na wagombea wengine wa CCM ili serikali iendelee kuboresha huduma za afya mkoani humo. Akizungumza mbele ya wananchi, Dkt. Samia ameahidi kuimarisha usambazaji wa dawa katika vituo vya afya .
Mhe. Samia ameahidi kujenga vituo vya afya katika maeneo ya Litolo na Mchomoro sambamba na kununua gari la kubebea wagonjwa ili kurahisisha huduma za dharura, na kukamilisha Hospitali ya Rufaa ya Ruvuma.
Katika hatua nyingine ameahidi kusogeza huduma za kibingwa karibu na wananchi ambapo ameahidi kukamilisha ujenzi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma ambayo itakuwa inatoa huduma za kibingwa moja kwa moja mkoani humo, ili wananchi wasilazimike kusafiri mbali kufuata matibabu ya kibingwa.

