NANYUMBU WAWEKA KIBINDONI BIL 73 ZA KOROSHO

Published:

                                 

DKT Samia aahidi kuhusu  Kilimo Bora na Maisha Bora Kwa Wakulima-MTWARA

Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akihutubia wananchi wa Mangaka wilaya ya Nanyumbu akisisitiza mafanikio yaliyopatikana kupitia ruzuku za pembejeo na mbolea. Ameeleza kuwa matumizi bora ya ruzuku yamewezesha ongezeko kubwa la uzalishaji wa mazao ya biashara na chakula.

Aidha, akielezea , uzalishaji wa korosho umeongezeka kutoka tani 15,000 hadi tani 24,000, na kuwaingizia wakulima zaidi ya shilingi bilioni 73. Mazao mengine kama karanga yameongezeka Tani 26,100 yenye thamani bilioni 65 hadi tani 33,170 yenye thamani ya bilioni 82.9, ufuta umeongezeka kutoka tani 1,580 yenye thamani ya bilioni 3.9 hadi tani 11,800 yenye thamani ya bilioni 38.8. na zao la mbaazi limeongezeka  kutoka tani 1,130 yenye thamani ya bilioni 1 hadi 5,950 bilioni 10 na milioni 800 zimeingia mkononi kwa wakulima. Dkt. Samia amesisitiza kuwa mafanikio haya yamewawezesha wananchi kujenga nyumba bora, kusomesha watoto na kuimarisha maisha yao.

Aidha, miradi ya visima vya umwagiliaji katika maeneo ya Likokona, Lukula na Masugulu ipo hatua za mwisho ili kuongeza uzalishaji wa mazao kwa kilimo cha umwagiliaji.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img