BENKI YA DUNIA: KILA DOLA MOJA INAYOWEKEZWA KWENYE BIMA YA AFYA HUCHANGIA HADI DOLA 5 KWENYE PATO LA TAIFA (GDP)

Published:

Dkt Samia ameahidi Bima ya Afya kwa Wote (Universal Health Coverage) kuanza ndani ya siku 100 baada ya kuapishwa ikiwa atachaguliwa Oktoba 29.

Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, kila dola 1 inayowekezwa kwenye bima ya afya huleta faida ya hadi dola 5 kwa uchumi kupitia kuongezeka kwa tija ya kazi, kupungua kwa siku za kazi zilizopotea (utoro kazini )

Katika kutekeleza ahadi za siku 100 ya kuanzisha rasmi Mfumo wa Taifa wa Bima ya Afya kwa Wote, Serikali inalenga kuwahudumia makundi maalum yenye uhitaji mkubwa wa huduma za afya wazee, watoto, mama wajawazito na watu wenye ulemavu ambao kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 wanachangia sehemu kubwa ya Watanzania milioni 61.7. Takriban asilimia 65.1 ya Watanzania hao wanaishi vijijini ambako huduma za afya ni changamoto.

Takwimu zinaonyesha kuwa ni asilimia 7 tu ya Watanzania waliokuwa na bima ya afya kufikia mwaka huo, hali inayodhihirisha pengo kubwa la upatikanaji wa huduma bora.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img